Nyumba Zangu

Simamia nyumba zako bila daftari

Wapangaji, mikataba na kodi mahali pamoja. Jua nani amelipa, nani anadaiwa, na unadai kiasi gani — kwa mguso mmoja.

Dashibodi ya mwenye nyumba Ukusanyaji wa kodi
Vipengele

Kila kitu unachohitaji, sehemu moja

Imetengenezwa kwa ajili ya wamiliki wa nyumba Tanzania — kwa Kiswahili, na kwa jinsi biashara inavyofanyika hapa.

🏠

Nyumba na vyumba

Nyumba za kawaida, apartment, maduka, ofisi na compound. Kila chumba na kodi yake.

👥

Wapangaji

Wamepangwa kwa nyumba. Piga simu au tuma WhatsApp moja kwa moja kutoka kwenye app.

📄

Mikataba ya kidijitali

Tengeneza, saini na hifadhi mkataba ndani ya app. Hakuna karatasi wala kupoteza nakala.

🧾

Kumbukumbu za kodi

Rekodi malipo, toa risiti yenye namba, na fuatilia madeni kwa kila mpangaji.

🔧

Matengenezo

Mpangaji anatuma ombi, wewe unaona na kubadilisha hali hadi limekamilika.

🔔

Mikataba inayoisha

App inakukumbusha kabla mkataba haujaisha — siku 30, 15, 7 na 3.

Kodi

Jua nani amelipa, papo hapo

  • Rekodi malipo kwa taslimu, M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au benki
  • Malipo ya sehemu yanakubalika — salio linabaki likidaiwa
  • Risiti yenye namba ya kipekee, unamtumia mpangaji kwa WhatsApp
  • Kumbusho la kodi kwa wasiolipa — kitufe kimoja, ujumbe umeshaandikwa
  • Kiwango cha ukusanyaji kwa kila mwezi, na madeni ya nyuma
App haipokei pesa.

Wewe na mpangaji mnalipana kama mlivyozoea. App inatunza kumbukumbu tu — ndiyo maana ni rahisi na salama.

Ukurasa wa ukusanyaji wa kodi
Risiti ya malipo
Kwa mpangaji

Mpangaji naye ana app yake

Si mwenye nyumba pekee. Mpangaji anaingia kwa akaunti yake na kuona mambo yake mwenyewe.

  • Ona mkataba wake na kuusaini kidijitali
  • Ona risiti za kodi alizolipa na deni lake
  • Omba matengenezo — maji, umeme, mlango
  • Omba kuongeza mkataba unapokaribia kuisha
  • Hifadhi nyaraka zake — kitambulisho, mkataba, picha
Anza leo

Nyumba Zangu ni bure kuanza

Pakua, ongeza nyumba yako ya kwanza, kisha waalike wapangaji wako.

Pata kwenye Google Play Wasiliana nasi